Episode 14: KISASI CHA DAMU
Giza nene lilikuwa limetanda ndani ya buti la gari, huku harufu ya mafuta ya gari na vumbi ikimfanya Aisha ahisi kukosa pumzi. Kila gari lilipogonga shimo, Aisha alihisi maumivu makali kwenye mshono wake wa zamani, kana kwamba unachanika upya. Alijaribu kutoa sauti, lakini ulimi wake ulikuwa mzito kutokana na yale maji aliyopewa na Anita.
Gari lilisimama katikati ya pori moja huko maeneo ya kando kando ya mji wa Bagamoyo. Milango ilifunguka, na mwanga wa tochi ulimmulika Aisha machoni, ukimfanya afumbe macho kwa maumivu. Nasra alisimama mbele yake, akiwa ameshika kisu kidogo chenye makali na chupa ya mafuta ya ajabu.
"Mshusheni," Nasra aliamuru kwa sauti ya baridi iliyopasua ukimya wa usiku.
Wanaume wawili walimvuta Aisha na kumtupa kwenye nyasi kavu. Aisha alijitahidi kujikokota kwa magoti, akijaribu kumshika Nasra miguu yake. "Dada... nisamehe... nilipotea dada yangu... shetani alinipitia," Aisha alinong'ona huku akilia kwa uchungu, machozi yakichanganyika na mchanga.
Nasra alicheka kicheko kilichojaa dhihaka, kisha akamshika Aisha kidevu na kumwinua juu. "Shetani hakukupitia Aisha, wewe ndiye uliyekuwa shetani. Ulizama kwenye mikono ya mume wangu ukidhani mimi ni mjinga. Ulikula raha wakati mimi nalia gerezani, ukitumia mali zangu na mwili wangu."
Nasra alizungusha kisu kile karibu na uso wa Aisha. "Ulijua Abdul amekufa? Ameacha kila kitu kwangu. Lakini kabla hajafa, aliniambia nikupe zawadi ya mwisho."
Nasra alimpasulia Aisha ile kanga aliyokuwa ameivaa, akionyesha lile kovu la upasuaji lililokuwa tumboni mwake. "Hapa ndipo palipokuwa na uzao wa mume wangu? Hapa ndipo mlipochezea dhambi yenu?" Nasra alianza kupaka yale mafuta ya kienyeji juu ya lile kovu la Aisha, huku akisoma maneno ya kutisha.
Ghafla, Aisha alianza kuhisi joto kali sana tumboni mwake, kana kwamba amemwagiwa makaa ya moto. Alipiga yowe la kutisha lililosikika kote porini. Mwili wake ulianza kutoa moshi mwembamba, na kila mahali alipokuwa akishikwa na Abdul wakati wa tendo la ndoa, palianza kutoa vidonda vibaya vilivyokuwa vikitoa usaha papo hapo.
"Huu ndio ushahidi wa usaliti wako, Aisha. Kila mguso wa mwanamume utakuwa kwako ni adhabu. Utazurura mitaani ukiwa na uzuri wako wa nje, lakini ndani utakuwa unaoza. Hakuna mwanamume atakayeweza kukukaribia bila kukimbia harufu yako!"
Nasra alimwacha Aisha akivuma kwa maumivu makali. Aligeuka na kupanda ndani ya gari, akimwacha mdogo wake katikati ya pori, uchi na mwenye vidonda vilivyoanza kuvutia nzi wa usiku.
"Dada! Usiniache hapa! Dadaaa!" Aisha alipiga kelele, lakini gari liliondoka kwa kasi, likiacha vumbi lililoziba macho yake.
Aisha alibaki akigaagaa kwenye majani, huku akishika tumbo lake ambalo sasa lilikuwa na harufu ya kifo. Kila alipojaribu kusimama, alihisi nguvu zinamuishia. Katika hali ile ya nusu kifo, aliona kivuli cha Abdul kikisimama mbele yake, kikimcheka dharau.
Lakini katikati ya giza lile, mwanga wa gari lingine ulitokea kwa mbali. Je, ni wasamaria wema, au ni mwanzo wa adhabu nyingine mbaya zaidi kwa binti huyu aliyepotea kwa tamaa?
---
**Itaendelea Sehemu ya 15 (EPISODE YA MWISHO)...**