✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 21: KUZALIWA KWA SHETANI NA MOTO WA HOSPITALI

Ray aliingia ndani ya chumba cha upasuaji kwa kishindo, mlango wa chuma ukajikunja kana kwamba umesukumwa na upepo wa dhoruba. Harufu ya damu iliyochanganyika na kiberiti ilijaza chumba kile. Madaktari na wauguzi walikuwa wamejishika pembeni, wakiwa wameparalaiti kwa hofu, huku wakishuhudia tukio ambalo halikuwahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Rose alikuwa amekaa katikati ya kitanda cha upasuaji, miguu yake iliyooza ikining’inia, huku tumbo lake likipasuka taratibu. Hakukuwa na damu ya kawaida; badala yake, utelezi mweusi ulikuwa ukitoka katikati ya mapaja yake. Rose alikuwa akicheka huku akirarua ngozi ya tumbo lake mwenyewe kwa kucha zake ndefu.

"Ray! Tazama mwanao!" Rose alipiga kelele, sauti yake ikiwa imepasuka.

Ghafla, kiumbe cha ajabu kilichomoza kutoka tumboni mwa Rose. Hakikuwa na ngozi, nyama yake ilikuwa nyekundu mbichi, na badala ya kulia kama mtoto, kilitoa muungurumo wa simba. Macho yake yalikuwa mawili makubwa ya moto yaliyokuwa yakimtazama Ray kwa kiu ya damu. Kile kiumbe kilikuwa na mikono mirefu yenye kucha za chuma, na mara tu kilipogusa hewa ya hospitali, vifaa vyote vya umeme vilianza kulipuka.

*"Boom! Spark! Boom!"*

Moto wa ajabu, wenye rangi ya kijani na bluu, ulianza kushika kwenye mapazia na vitanda. Ray alishika kile kisu cha shaba alichopewa na Bibi Ma-Mkunde, mkono wake ukitetemeka. Alimtazama Rose—mwanamke aliyewahi kumpenda, mwanamke aliyepanga kufunga naye ndoa—sasa amekuwa chombo cha shetani.

"Ray, usiniue... tafadhali," Rose alisema kwa sauti yake ya asili kwa sekunde moja, machozi ya damu yakimtoka. "Niokoe Ray..."

Lakini kile kiumbe kilichokuwa kifuani mwake kilimvuta Rose na kuanza kunyonya uhai wake. Rose alianza kukauka kama jani lililopigwa na jua, ngozi yake ikishikana na mifupa. Ray alijua akisita kwa sekunde moja zaidi, kile kiumbe kingekuwa na nguvu kamili na kuanza kuua kila mtu hospitalini hapo.

"Nisamehe Rose, lakini hili ndilo deni la usaliti wetu!" Ray alipiga yowe, akijitupa mbele huku kisu cha shaba kikimulika mwanga mkali.

Ray alikichoma kile kiumbe katikati ya kifua chake, pale ambapo moyo wa moto ulikuwa ukidunda. Mlio wa kutisha ulisikika, sauti ya kiumbe hicho ikichanganyika na sauti ya Nasma iliyokuwa ikilaani kutoka ulimwengu mwingine. Moto ulizidi kuwa mkubwa, ukizunguka miili yao watatu—Ray, Rose, na kile kiumbe cha laana.

Hospitali ilianza kuporomoka. Wagonjwa na madaktari walikimbia nje huku wakiona moshi mweusi ukipanda angani. Bibi Ma-Mkunde alisimama nje, akitazama lile jengo likiteketea, huku akijua kuwa ndani ya ule moto, kuna kitu kimoja tu kinachoweza kutoka kikiwa hai.

"Ray! Toka!" Bibi alipiga kelele, lakini jengo liliporomoka kwa kishindo kikubwa, likizika siri zote, laana zote, na usaliti wote chini ya vifusi vya moto.

---

**Katika Sehemu ya 22 (HITIMISHO):** Wiki mbili baadaye, kijiji cha Mwanga kimetulia, lakini kuna kaburi moja ambalo halina jina lililopo pembezoni mwa msitu. Ray anaonekana akitembea peke yake kuelekea kusikojulikana, huku akiwa amebeba siri nzito moyoni mwake. Je, Nasma amekufa kweli? Na nini kilitokea kwa lile kiumbe?

**Usikose: SEHEMU YA 22: MAJIVU YA AGANO (TAMATI)**