✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 2: Mpaka wa Hatari

Kelvin alihisi kijasho jembamba kikimvunja. Alimtazama Briana, ambaye sasa alikuwa ameelekeza macho yake moja kwa moja kwenye macho ya Kelvin, akionekana kutotikisika hata chembe. Katika umri wake wa miaka kumi na saba, Briana alikuwa na ujasiri uliomshinda hata Kelvin mwenye miaka ishirini na tano.

"Briana, rudi darasani," Kelvin alisema kwa sauti iliyokuwa ikitetemeka kidogo, akijaribu kupanga karatasi zilizokuwa mezani kwake ili kuficha mshtuko wake. "Una mtihani wa taifa baada ya miezi michache. Haya mambo unayoyawaza hayatakusaidia kupata daraja la kwanza."

Briana alicheka kicheko kifupi cha kimahaba, kisha akasogea hatua moja zaidi mbele. "Mwalimu, daraja la kwanza nitapata, lakini nitapata wapi mwalimu mwingine kama wewe? Unajua kabisa kuwa tangu uingie shule hii, kila msichana anatamani kuwa karibu nawe. Lakini mimi... mimi sitaki tu kuwa karibu, nataka uwe wangu."

Maneno hayo yalikuwa kama msumari wa moto kwa Kelvin. Alijua fika kuwa mchezo huu ni hatari—ukigundulika, ni mwisho wa kazi yake na pengine kifungo jela. Lakini urembo wa Briana na jinsi alivyokuwa akijitolea kwake vilikuwa vimeanza kubomoa ukuta wa ulinzi alioujenga moyoni mwake.

Ghafla, mlango wa ofisi ulifunguka. Mwalimu Vincent, mwalimu mkuu msaidizi ambaye alikuwa na sifa ya ukali na ufuatiliaji, aliingia ndani. Kelvin na Briana walishtuka na kutengana haraka. Macho ya Mwalimu Vincent yalikuwa na shaka, yakihama kutoka kwa Kelvin kwenda kwa Briana.

"Kuna nini hapa?" Vincent aliuliza kwa sauti ya mamlaka, huku akimtazama Briana kwa ukali. "Mwanafunzi unafanya nini ofisini kwa mwalimu kijana wakati huu wa masomo?"

**Inaendelea Episode 3...**