Episode 6: Mapigo ya Moyo
Baada ya kishindo cha hatua za Mwalimu Vincent kufifia, Kelvin alifunga mlango wake kwa kufuli na kuegemea mbao za mlango huku akihema kwa nguvu. Chumba kilikuwa kimya, isipokuwa sauti ya mbali ya mlinzi akiendelea kupiga upatu kule upande wa madarasa.
"Briana, toka," Kelvin alinong'ona.
Briana alijivuta kutoka uvunguni, nywele zake zikiwa zimevurugika kidogo na mavumbi ya sakafuni yakionekana kwenye mtandio wake. Macho yake yalikuwa yamejaa hofu, lakini alipoona Kelvin yuko salama, alitabasamu kidogo—tabasamu ambalo liliashiria kuwa hata katika hatari ile, bado alikuwa na ujasiri wa ajabu.
"Umeona, Kelvin? Vincent ni hatari," Briana alisema akijipangusa mavumbi. "Ananitaka kwa nguvu, na asiponipata mimi, atakuangamiza wewe. Lazima tufanye kitu."
Kelvin alimshika Briana mabega, akimkazia macho. "Briana, husikii? Huyu mtu amekaribia kutufukuza kazi na shule usiku huu! Huwezi kubaki hapa hata sekunde moja zaidi. Lazima urudi bwenini sasa hivi kabla Vincent hajarudi hapa akijua kuwa alidanganywa na kivuli cha mlinzi."
"Lakini nitatoka vipi? Vincent yuko nje anazunguka," Briana aliuliza kwa wasiwasi.
Kelvin alichungulia dirishani. Aliona mwanga wa tochi kwa mbali ukielekea bwenini kwa wasichana. "Sikiliza, utapita njia ya nyuma ya maabara. Kuna tundu dogo kwenye uzio wa seng'enge ambalo ninalijua. Ukifika kule, rudi bwenini kimyakimya. Kesho darasani, usijaribu hata kunisogelea wala kunisemesha. Tutaishi kama watu tusiojuana kabisa."
Briana aliguna, kisha akasogea na kumshika Kelvin mkono. "Nitafanya hivyo, mwalimu wangu. Lakini kumbuka ahadi yako... hutaniacha peke yangu kwenye huu mtego wa Vincent, sawa?"
Kelvin alitikisa kichwa, ingawa moyoni alijua kuwa alikuwa ameshaingia kwenye mtego ambao huenda usingekuwa na mlango wa kutokea. Briana alitoka nje kama kivuli na kutokomea gizani.
Siku iliyofuata, Kelvin alifika darasani akiwa na uchovu mwingi. Alipoanza kufundisha, alishtuka kuona kiti cha Briana kikiwa wazi. Briana hakuwepo darasani. Badala yake, Mwalimu Vincent aliingia darasani hapo katikati ya kipindi akiwa na barua mkononi.
"Mwalimu Kelvin, naomba nikuone ofisini kwa Mkuu wa Shule sasa hivi," Vincent alisema kwa sauti ya baridi iliyosheheni ushindi. "Kuna mwanafunzi amekutwa na barua ya mapenzi... na jina lako limeandikwa humo."
**Inaendelea Episode 7...**