Episode 12: PAMBANO LA MWISHO (MWISHO WA AGANO)
Moyo wangu ulilipuka kwa hofu nilipoona picha ya mzee wa kovu akiwa nyumbani kwa Mama kijijini. Bila kupoteza muda, nilimvuta Kaka Godfrey aliyekuwa bado anatetemeka, na Grace ambaye alikuwa ndiyo kwanza anapata fahamu vizuri. Tuliingia kwenye gari pekee lililokuwa limebaki—gari langu la zamani ambalo halikuwa sehemu ya mali za agano la giza.
"Kaka, amka! Mama yuko hatarini!" nilimfokea Godfrey. Alistuka, machozi yakimtoka. Safari hii hakuwa mnyama tena, alikuwa kaka yangu aliyepotea na sasa anarudi kwenye utu.
Tulipofika kijijini saa tisa alasiri, hali ya hewa ilikuwa nzito. Nyumba ya Mama ilikuwa imezungukwa na ukungu mweusi, ingawa jua lilikuwa bado kali. Majirani walikuwa wamesimama mbali, wakiogopa kusogea.
Tulipoingia ndani ya fensi, tulimkuta mzee wa kovu ameketi katikati ya uwanja. Mbele yake kulikuwa na kile kioo cha dhahabu, na ndani yake, picha ya Mama ilikuwa inaanza kufifia, ikibadilishwa na sura ya mnyama wa ajabu. Mama alikuwa amelala chini, hajitambui, huku nyoka yule mweusi niliyemuona kwenye "Live Stream" akizunguka mwili wake.
"Mmerudi?" mzee wa kovu alicheka kicheko kilichotetemesha ardhi. "Agano halivunjwi na mzee wa kanzu mlimani. Agano linahitaji damu ya mlipaji. Godfrey ameshindwa, sasa mmoja wenu lazima achukue nafasi yake ndani ya kioo hiki."
Nilipiga hatua mbele, nikiwa nimeshika kile kisu cha fedha nilichokiiba. "Mimi nitachukua nafasi hiyo! Mwache Mama na Grace waende zao!" nilipiga kelele.
Lakini kabla sijasogea, Kaka Godfrey alinizuia. Aliniangalia kwa macho yaliyojawa na upendo ambao sikuuona kwa miaka ishirini. "Hapana mdogo wangu. Mimi ndiye niliyeleta laana hii. Mimi ndiye niliyemtoa Baba. Ni zamu yangu kulipa deni la familia."
Godfrey alikimbia kwa kasi ya ajabu na kujitosa kwenye kile kioo cha dhahabu kabla mzee wa kovu hajafanya lolote. Alikikumbatia kioo kile kwa nguvu zake zote.
"Baba! Nisamehe!" Godfrey alipiga kelele ya mwisho.
Mlipuko mkubwa wa moto mweusi ulitokea. Kioo cha dhahabu kilipasuka vipande maelfu. Mzee wa kovu alipiga kelele ya maumivu makali huku mwili wake ukianza kuyeyuka na kuwa vumbi. Nyoka mweusi alitokomea ardhini na ukungu wote ukatoweka.
Dakika chache baadaye, hali ilitulia. Mama alizinduka na kuanza kukohoa, akitazama huku na kule kwa mshangao. Grace alimkimbilia na kumkumbatia. Lakini Kaka Godfrey... Godfrey hakuwepo tena. Pale palipokuwa na kioo, palibaki majivu tu na kile kisu cha fedha.
Tulibaki pale tukilia, tukijua kuwa Godfrey amejitoa muhanga ili kufuta dhambi zake. Utajiri wote uliopatikana kwa damu ulitoweka; maduka yaligeuka majivu, magari yaliharibika, na akaunti za benki zilifungwa. Tulibaki masikini wa mali, lakini matajiri wa amani.
Siku ya pili, nikiwa nimekaa barazani kwa Mama, nilihisi baridi nyepesi ikipita. Niligeuka na kuona kivuli changu kimerudi sakafuni! Na pembeni yake, kulikuwa na vivuli viwili vikinisalimia kwa mbali—kivuli cha Baba na kivuli cha Kaka Godfrey, wakitembea kwa pamoja kuelekea kwenye nuru.
**MWISHO.**