✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 18: UTATA WA UTAWALA

Sebule ilikuwa imetapakaa mabaki ya agano lililopasuka. **Sam** alikuwa amelala sakafuni, akitweta kwa maumivu ya mwisho, mwili wake ukiwa umepoteza kila aina ya nguvu aliyokuwa akijivunia. **Bi. Rehema** na **Mwajuma** walikuwa wamejishika mashavu, miili yao ikiwa na malengelenge ya kuungua kutokana na sumu ya kijani iliyomlipukia mpenzi wao wa siri.

**Mzee Sura** alisimama katikati ya uchafu huo. Ingawa paji la uso wake lilikuwa na jasho na kiganja kikimvuja damu, macho yake hayakuwa na unyonge tena. Alikuwa mwanaume aliyepoteza "dude" lake, lakini alikuwa amerudisha nafsi yake.

"Inatosha!" Mzee Sura alinguruma, na safari hii sauti yake haikutetema. "Mwajuma, chukua maji na vitambaa usafishe huu uchafu. Rehema, nenda chumbani ukajifunge khanga vizuri na uache kulia."

Bi. Rehema alimtazama Sura kwa dharau iliyochanganyika na hofu. "Utatuamuru nini Sura? Wewe bado ni mlemavu. Sam ameshindwa, lakini hiyo haikufanyi wewe kuwa mwanaume tena mbele yetu."

Mzee Sura alimkaribia Bi. Rehema na kumshika kidevu kwa nguvu. "Mwanaume si kile kilichopo katikati ya miguu pekee, Rehema. Mwanaume ni yule anayeweza kuzuia nyumba yake isiteketeze uzao wake. Tazama huyu kiumbe," Sura alimnyooshea kidole yule mtoto wa ajabu aliyekuwa bado amesimama pembeni. "Huyu ni matunda ya uchafu wenu. Mnataka aendelee kukua kwenye damu na mafuta?"

Mwajuma, akitetemeka, alianza kufuta sakafu huku akimlenga Sam kwa mateke. "Shetani wewe Sam! Umemponza mume wetu, umetuponza na sisi!"

Sam alijaribu kunyanyua mkono wake, lakini ulikuwa mzito kama jiwe. "Sura... nisaidie..." alidonoa maneno kwa shida. "Kuna... kuna siri nyingine... kule nyuma ya nyumba... kwenye shimo la choo cha zamani..."

Sura alistuka. Alimkabidhi yule mtoto uzi mwekundu, kisha akatoka nje huku akichechemea. Bi. Rehema na Mwajuma walimfuata kwa nyuma, wakiwa na shauku na hofu ya nini kingine kimefichwa.

Kule nyuma ya nyumba, kwenye shimo la choo cha zamani ambalo lilikuwa limefunikwa na mbao zilizooza, kulikuwa na harufu nzito ya kemikali. Mzee Sura alichukua mti na kuanza kufukua. Alichokiona kilimfanya azibe pua: Kulikuwa na masanduku madogo manne ya chuma, yaliyounganishwa na mirija ya ajabu kuelekea chini ya ardhi.

"Ni nini hiki, Sura?" Mwajuma aliuliza akiziba pua.

"Hii ndiyo karakana ya Sam na Juma," Sura alijibu kwa uchungu. "Walikuwa wanatumia choo hiki kutengeneza yale mafuta na unga mweupe. Walijua harufu ya choo itaficha harufu ya dawa zao. Na nyinyi, wake zangu, mlikuwa wasambazaji wa sumu hii mtaani kwetu!"

Ghafla, mtoto wa ajabu alitokea na kurukia juu ya yale masanduku. Alianza kuyagonga-gonga, na kila alipogonga, sauti ya kishindo ilisikika chini ya ardhi.

"Mali ya agano itarudi ardhini!" mtoto alipiga kelele.

Ardhi ilianza kutetemeka. Shimo la choo lilianza kumeza kila kitu—masanduku, mbao, na hata ile mirija. Lakini jambo la kutisha ni kwamba, kadiri shimo lilivyokuwa likimeza uchafu ule, ndivyo Bi. Rehema na Mwajuma walivyokuwa wakihisi maumivu makali vifuani mwao. Walikuwa wameunganishwa na agano lile kwa damu.

"Sura! Tusaidie! Tunakufa!" Bi. Rehema alianguka chini, akishika kifua chake.

Mzee Sura alitazama kiganja chake chenye damu, kisha akamtazama mtoto. Alijua lazima atoe kitu kingine ili kuokoa maisha ya wanawake hawa, licha ya usaliti wao. Alichukua ule mnyororo mwekundu na kuufunga mwilini mwake, kisha akajitupa kwenye lile shimo linalomeza kila kitu.

"Sura! Hapana!" Mwajuma alipiga yowe.

Mzee Sura alitumbukia kwenye giza la shimo lile, akitaka kukata mirija ya mwisho ya agano ili wake zake waishi. Ndani ya shimo, alikutana na kitu ambacho hakukitegemea: Juma (Baba Naah) alikuwa huko, akiwa ameshika mashine ya ajabu, macho yake yakitazama giza.

**ITAENDELEA EPISODE YA 19: KUZIMU YA CHINI YA ARDHI**