Episode 1: HARUFU YA KIFO NA SHINIKIZO LA TAJI
Jua lilikuwa likizama upande wa magharibi wa Ufalme wa mbali wa Kalinga, likiacha rangi ya damu angani—rangi iliyoshabihiana na hali ya ndani ya Ikulu. Mfalme Mzee, **Mtemi Ngunguti**, alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi kilichochakaa, akikohoa kikohozi kilichokuwa kikirarua ukimya wa ukumbi ule mkubwa. Kila pumzi aliyovuta ilionekana kama ya mwisho.
Pembeni yake, binti yake pekee, **Ghazala**, alikuwa amepiga magoti. Ghazala alikuwa mrembo kama mbalamwezi, mwenye ngozi laini iliyong’aa kwa mafuta ya nazi, lakini macho yake yalikuwa yamejaa mawingu ya hofu.
"Mwanangu," Mtemi alizungumza kwa sauti ya mkwaruzo, "Ufalme huu ni kama mti mzee. Bila mizizi ya kiume, utaanguka na kuliwa na mchwa wa falme jirani."
Wazee wa baraza, wakiwa wamejifunga magome ya miti na shanga shingoni, walikuwa wakishonana kwa maneno ya chini kwa chini. Sheria ya Kalinga haikuwa na huruma: *Kiti cha enzi hakikaliwi na mwanamke.* Ili kumlinda Ghazala asinyang’anywe mamlaka na wavamizi, ilibidi apatikane mwanaume shujaa kutoka ndani ya ufalme huo atakayepewa binti huyo na kuwa mfalme.
Siku ya mchujo ilifika. Mto **Sangu**, mto unaotiririka maji ya kijani yaliyojaa mamba wakubwa wenye njaa, ulikuwa ndio uwanja wa majaribio. Mamia ya wanakijiji walijaa kingoni. Kelele za ngoma na vigelegele vilitawala, lakini mioyo ya vijana washindani ilikuwa ikidunda kama nyundo.
Miongoni mwa umati, alikuwepo kijana mmoja, **Kaisi**. Alikuwa kijana mnyonge, aliyezoea jembe na vibarua vya mashamba ya watu baada ya wazazi wake kufariki. Alikuwa amesimama kando, akishangaa ujasiri wa wale vijana watano waliobaki kwenye fainali. Kaisi hakuwa na ndoto ya ufalme; yeye alikuwa akitafuta tu namna ya kupata mlo wa jioni.
Mtemi Ngunguti alisimama kwa tabu, akanyoosha mkono wake uliokuwa ukitetemeka kuelekea mtoni. "Yeyote atakayevuka kwenda upande wa pili na kurudi akiwa hai, huyo ndiye atakayemshika mkono Ghazala. Huyo ndiye atakayekuwa simba wa Kalinga!"
Mamba walionekana wakichomoza macho yao juu ya maji, wakisubiri karamu. Wale vijana watano, "mashujaa" waliosifika, walirudi nyuma kwa uoga. Jasho liliwatoka. Mmoja alidondoka kwa kutetemeka magoti.
"Hamna mwanaume ndani ya ardhi hii?" Mtemi alifoka kwa hasira. "Uongozi hauhitaji muoga! Kama mmeshindwa kuogelea, basi ufalme huu umekufa!"
Kabla Mtemi ajamaliza neno lake, gafla... **PAAA!**
Mlio mkubwa wa kitu kilichotumbukia majini ulisikika. Kaisi, ambaye alikuwa amesimama karibu na mshindani mmoja aliyekuwa akitetemeka, alijikuta akipoteza usawa. Yule mshindani, kwa hofu na kujihami asidondoke yeye, alimnyooshea Kaisi mkono wa nguvu na kumsukuma kwa bahati mbaya.
Maji ya baridi yalimpokea Kaisi. Kelele za wanakijiji zilikuwa kama radi.
"Anavuka! Tazama, kijana anavuka!"
Kaisi hakusikia sifa zao. Macho yake yalikutana na mamba mkubwa aliyekuwa akija kwa kasi ya mshale. Alijua hapa ni kifo au maisha. Alianza kupiga mbizi kwa nguvu ya ajabu, mikono yake ikirarua maji kama kasia la mashua iliyopata dhoruba.
Wakati akikaribia katikati ya mto, mamba mmoja alizama na kutokea chini yake. Kaisi alihisi maumivu makali, maumivu yaliyopitiliza uwezo wa binadamu kuvumilia. Alihisi meno ya msumeno yakimkata sehemu yake ya siri kwa nguvu ya ajabu. Damu nyekundu ilianza kuchafua maji ya kijani.
Kwa hasira ya maumivu na msukumo wa kifo, Kaisi alitumia mguu wake wa kushoto kumpiga mamba yule na kupiga mbizi ya mwisho kuelekea upande wa pili. Alitokea ng’ambo nyingine akitapatapa.
Wanakijiji walilipuka kwa makofi na vigelegele. "Mfalme! Mfalme amepatikana!"
Lakini upande wa pili, Kaisi hakuwa anasherehekea. Alikuwa akilia kwa uchungu wa moyo na mwili. Alishika sehemu yake ya siri iliyokuwa ikitiririka damu mfululizo; kile chombo chake cha kiume kilikuwa kimepotea mdomoni mwa mamba. Kwa hofu ya kuonekana vile, alijivuta na kukimbilia porini, akiacha alama ya damu kwenye majani, huku nyuma yake walinzi wa mfalme wakianza kumfuata kwa kasi.
Hatima yake sasa ilikuwa mikononi mwa giza la pori na mganga mmoja wa ajabu aliyekuwa akiishi huko...
**ITAENDELEA EPISODE 2: TABIBU WA MSITU WA GIZA**