โœฆ Matangazo โœฆ

๐Ÿ“– Story Tamu

Episode 12: Mchezo wa Kivuli

Baraka alihisi kama yuko kwenye filamu ya kusisimua, lakini hii ilikuwa damu na nyama. Lisa alikuwa akigonga keyboard ya laptop yake kwa kasi ya ajabu, mwanga wa kioo ukiakisi kwenye macho yake yaliyojaa hofu.

"Baraka, angalia hapa," Lisa alisema kwa sauti ya kukata tamaa. "Hii siyo Telegram tu. Video yako imepandishwa kwenye *Dark Web*. Wameiweka kama 'Premium Content'. Watu wanailipia kwa kutumia Bitcoin ili kuona kile walichokiita 'The Managerโ€™s Fall'."

Baraka alitazama kioo cha laptop. Alijiona akiwa uchi, uso wake ukiwa wazi kabisa, huku maandishi ya lugha ngeni yakizunguka pembeni. Alihisi kichefuchefu. "Lisa, fanya lolote. Ifute. Naomba uifute!"

"Siwezi kuifuta moja kwa moja kutoka hapa, Baraka. Lazima niingie kwenye 'Admin Panel' ya huyu anayejiita 'Mwenye Nyumba'. Na siri ya kuingia huko iko kwenye 'Password' ambayo Sasha aliificha kwenye picha moja aliyokutumia. Unaikumbuka picha ya kwanza kabisa aliyokutumia?"

Wakati Baraka akijaribu kukumbuka, simu yake ilianza kuita. Safari hii ilikuwa namba ya Frank, shemeji yake. Baraka alipokea kwa haraka.

"Baraka! Baraka, amevunja gari!" Frank alikuwa akipiga kelele, sauti yake ikiwa na mwangwi wa upepo na ving'ora.

"Nani? Nini kimetokea Frank?"

"Sasha! Alikuwa kwenye karandinga la polisi kuelekea mahakamani. Gari limevamiwa na watu wenye silaha hapa karibu na Salender Bridge. Wameua askari wawili na kumtorosha Sasha! Baraka, kimbia! Atakuja kwako!"

Baraka alidondosha simu. Alimgeukia Lisa ambaye naye alikuwa amesikia kila kitu. "Lisa, lazima tuondoke hapa sasa hivi!"

Walizima taa zote na kuchukua laptop. Lakini kabla hawajafika mlangoni, walisikia mlio wa breki kali nje ya nyumba ya Baraka. Gari jeusi lilikuwa limeegeshwa, na milango ikafunguka kwa kishindo.

"Wamefika," Lisa alinong'ona kwa sauti iliyolowa hofu.

Baraka alimvuta Lisa kuelekea chumbani na kujifungia. Baada ya sekunde chache, walisikia mlango wa mbele ukivunjwa. Hatua za viatu vya juu (high heels) zilisikika zikitembea taratibu kwenye sakafu ya sebule. Hatua zile zilikuwa na mdundo ambao Baraka aliujua vyema.

"Baraka... mpenzi wangu..." Sauti ya Sasha iliita kwa upole, lakini ilikuwa na ukatili ulioshindwa kufichika. "Najua uko humu. Usijifiche. Nimekuja kukupa 'bonus' ya video yetu ya mwisho kabla sijaondoka nchini."

Baraka alishika kisu chake kwa nguvu. Sasha alifika mlangoni mwa chumba na kugonga mara tatu. "Fungua mpenzi, au nitamfanya Lisa kile nilichomfanya Dr. Steven. Najua yuko hapo na laptop yake."

Baraka alimashiria Lisa ajifiche chini ya kitandani. Kisha, kwa ujasiri wa mwisho, Baraka alifungua mlango.

Sasha alikuwa amesimama hapo. Alikuwa bado amevaa lile koti la hospitali, lakini lilikuwa na madoa ya damu. Macho yake yalikuwa yakimetameta kwa wazimu. Alishika bastola ndogo mkononi mwake, na mkono mwingine ulikuwa umeshika chupa ya champagne.

"Mshangao!" Sasha alicheka, kisha akamsukuma Baraka ndani na kufunga mlango kwa teke. Alimkaribia Baraka na kuanza kumvua shati kwa ncha ya bastola. "Watu wanataka kuona 'The Manager' akifa akiwa anafurahia penzi langu kwa mara ya mwisho. Washa kamera ya laptop yako, Lisa! Najua uko hapo chini."

Sasha alijitupa kitandani na kumlaza Baraka kwa nguvu, akimkalia kifuani huku akielekeza bastola kwenye kidevu chake. "Leo, haturekodi kwa ajili ya pesa, Baraka. Tunarekodi kwa ajili ya kifo. Na dunia nzima itatazama jinsi unavyokata roho ukiwa ndani ya Nurse wako mpendwa."

---

**Katika Episode ya kumi na tatu:**
Sasha anaanza kufanya kitendo cha unyama huku akilazimisha Lisa kurusha tukio hilo mubashara (Live Stream) kwenye mtandao wa giza. Lakini Baraka anagundua udhaifu mmoja wa Sasha uliopo kwenye jeraha lake la zamani.

**Usikose EPISODE 13: "Kifo Mubashara"**