Episode 10: WIZI WA KANISANI
Muda ulikuwa unayoyoma kwa kasi ya ajabu. Neema alishaanza kuelekea shuleni huku akinitolea ulimi wa dharau, akijua kanishika pabaya. Nilijua fika kuwa Mama ni mtu wa nidhamu, na lile bahasha la michango ya kanisani kwake ni kitu kitakatifu. Akilikabidhi kwa Mchungaji na kukutwa ile CD, sitakuwa na pa kutokea.
Nilirudi ndani ya nyumba huku nikijifanya natafuta soksi zangu zilizopotea. Mama alikuwa chumbani kwake akimalizia kuvaa kilemba chake cha kanisani, tayari kwa kikao cha saa nane. Nilichungulia kupitia upenyu wa mlango wa chumba cha wazazi; lile bahasha kubwa la kaki lilikuwa limetulia juu ya meza ya kioo, pembeni ya Biblia ya Mama.
*"Mwanangu, mbona bado huna haraka ya kwenda tuition? Saa mbili hiyo,"* sauti ya Mama ilinitikisa nikiwa mlangoni.
*"Mama, naona nimepoteza daftari langu la hesabu, nahisi niliacha hapa sebuleni jana,"* nilidanganya huku nikianza kupekua magazeti ya Mzee ili kuhamisha umakini wake.
Mama alitoka chumbani na kuelekea jikoni kunywa maji. Huu ndio ulikuwa upenyo wangu! Nilipenya ndani ya chumba cha wazazi kama kivuli. Mikono ilikuwa inatetemeka nikiishika ile bahasha ya kaki. Nilihisi kitu kigumu ndani yakeโndiyo yenyewe! Ile CD ya aibu ilikuwa imetulia katikati ya risiti za kanisani.
Niliingiza mkono kwa tahadhari ili niitoe, lakini ghafla nilisikia sauti ya Baba ikikaribia barazani akitokea kufuata funguo zake za ofisi alizozisahau.
*"Mama Neema! Umeona funguo zangu hapo sebuleni?"* Baba aliita huku akisukuma mlango wa nje.
Niliishiwa nguvu. Nikiwa nimeishika ile bahasha, sikuwa na muda wa kuitoa ile CD na kuirudisha bahasha mezani. Niliamua kufanya kitu cha hatari zaidi: Niliibeba bahasha nzima na kuificha ndani ya shati langu, kifuani, kisha nikaruka na kujificha nyuma ya mlango wa chumba cha wazazi.
Baba aliingia chumbani, akazunguka mara mbili kutafuta funguo, akazichukua juu ya kabati na kuondoka. Nilipumua kwa kishindo, lakini kabla sijatoka, Mama naye akaingia chumbani kuchukua lile bahasha tayari kwa safari ya kanisani.
Alitazama mezani. Akatama tena. *"Mungu wangu! Bahasha la michango liko wapi? Nimeliacha hapa sasa hivi!"* Mama alianza kupiga kelele kwa hofu, akidhani shetani amemchezea mchezo mbaya.
Nikiwa nimeganda nyuma ya mlango, nilihisi lile bahasha linaanza kuteleza kifuani mwangu. Kama likianguka sakafuni sasa hivi, nitaitwaje? Mwizi wa fedha za kanisani au mtazamaji wa picha za aibu? Kila upande ulikuwa na adhabu ya moto.
Mama alianza kusogea karibu na mlango nilipojificha, akitaka kuangalia kama bahasha limeanguka nyuma ya mlango. Nilijua sekunde tano zijazo, maisha yangu yanakwenda kubadilika milele.
**ITAENDELEA...**
---
**Episode 11 Inakuja: "MBINU YA KIPANGA"**