Episode 7: SUMU YA USALITI
Nasra alihisi dunia inazunguka. Ile mistari miwili mekundu kwenye kile kipimo ilikuwa kama hukumu ya kifo kwa ndoa yake. Alikishika kile kijiti kwa nguvu kiasi cha kutaka kukivunja, huku akimtazama mdogo wake, Aisha, aliyekuwa amelala fofofo kwa amani, hajui kuwa siri yake mbaya zaidi imegundulika.
Nasra alirudi chumbani kwake akiwa kama mwendawazimu. Alimlazama Abdul aliyekuwa akikoroma kwa amani, akajihisi kichefuchefu. "Huyu ndiye mwanamume niliyemwamini? Huyu ndiye mdogo wangu niliyemlea?" alinong'ona huku akiuma kucha zake mpaka damu ikatoka. Hakulala usiku kucha; alikuwa akipanga kisasi kitakachowaacha wote na kovu la maisha.
Asubuhi ilipofika, hali ya nyumba ilikuwa na ukimya wa kutisha. Abdul aliamka na kuwahi kazini ili kukwepa macho ya Nasra, huku Aisha akijivuta kutoka kitandani akiwa na uchovu wa hali ya juu.
"Mdogo wangu, leo mbona unachelewa kuamka? Unaumwa nini?" Nasra aliuliza kwa sauti tamu ya dhihaka wakati Aisha akitoka chumbani.
"Ni uchovu tu dada, kichwa kinaniuma kidogo," Aisha alijibu huku akijishika ukuta, akijaribu kuzuia kichefuchefu kisimrudie mbele ya dada yake.
Nasra alitabasamu, tabasamu ambalo halikufika machoni. "Basi usijali. Leo nimeamua kukupikia kitu maalum cha kukupa nguvu. Nenda kapumzike sebuleni, nitakuletea juisi ya baridi na chakula kizuri."
Aisha alishangaa ukarimu ule wa ghafla, lakini alishukuru na kwenda kukaa sebuleni. Alijilaza kwenye kochi lile lile ambalo siku chache zilizopita yeye na Abdul walikuwa wakifanya madhambi yao. Alikumbuka jinsi Abdul alivyokuwa akimnywesha mate na kumpapasa, akajikuta akitabasamu kwa siri huku akishika tumbo lake. "Mwanangu, baba yako anakupenda," aliwaza.
Wakati huo jikoni, Nasra alikuwa akitayarisha juisi ya maembe. Alichukua chupa ndogo ya dawa ya kuua wadudu (sumu) aliyokuwa ameificha kwenye kabati la vyombo. "Mlitaka kunipa uchungu? Basi onjeni uchungu huu," alinong'ona huku akidondosha matone kadhaa ya ile sumu ndani ya glasi ya Aisha. Hakutaka kumuua, alitaka kumfundisha adabu yeye na hicho kilichopo tumboni mwake.
Alitoka na glasi ile, akaikabidhi kwa Aisha kwa mikono inayoteteka kidogo. "Kunywa hii mdogo wangu, itakupa nguvu."
Aisha aliipokea na kuinywa yote kwa mkupuo mmoja kutokana na kiu na joto la Dar. "Asante dada, imepoa vizuri."
Hazikupita dakika kumi, Aisha alianza kuhisi mabadiliko. Tumbo lilianza kumkata kama anachanwa na wembe. "Dada... tumbo... nakufa dada!" Aisha alipiga yowe huku akijiviringisha sakafuni. Jasho la baridi lilimtokata, na ghafla akaanza kutapika mchanganyiko wa ile juisi na damu nyepesi.
Nasra alibaki amesimama, akimtazama mdogo wake kwa macho yaliyopagawa. "Huo ndio utamu wa mume wangu, Aisha! Hiyo ndiyo zawadi ya kunisaliti!" alimfokea huku akicheka kicheko cha kishirikina.
Aisha alikuwa hawezi tena kuongea. Alikuwa akipumulia juu juu, huku damu ikianza kutiririka kwenye miguu yake, ikichafua lile kochi la thamani. Kwa mbali, mlio wa gari la Abdul ulisikika getini; alikuwa amerudi kuchukua baadhi ya nyaraka alizozisahau.
Abdul aliingia ndani na kukutana na tukio la kutisha. Aisha yupo chini anagalagala kwenye damu, na Nasra amesimama pembeni akiwa ameshika ile glasi, uso wake ukiwa na tabasamu la kutisha.
"Nasra! Umefanya nini?!" Abdul alipiga yowe akimkimbilia Aisha.
"Nimempa anachostahili, Abdul! Na wewe unafuata!" Nasra alimrushia ile glasi ya kauri usoni.
---
**Itaendelea Sehemu ya 08...**