Episode 12: MGANGA WA BUGURUNI NA KAFARA YA DAMU
Vichochoro vya Buguruni vilikuwa na harufu ya maji machafu na moshi wa kuku wa choma, lakini harufu ya Lailah ilikuwa kali zaidi. Alijikaza, akijivuta huku akichechemea mpaka alipofika kwenye nyumba moja iliyochakaa, yenye mlango wa gunia.
"Ingia, binti uliyetupa lulu yako kwa nguruwe," sauti ya kikwaru ilisikika kutoka ndani ya giza.
Ndani kulikuwa na harufu ya udi, damu ya kuku, na mizizi iliyooza. Mganga mmoja aliyekuwa na jicho moja tu, Sheikh Sharifu, alikuwa amekaa kwenye mkeka wa kizamani. Alimtazama Lailah na kuanza kucheka kicheko cha kishirikina.
"Umechelewa, Lailah. Yule mzee wa madini hajachukua uzuri wako tu, amekupa 'kivuli cha mfu'. Kila unachogusa kitanyauka, na kila anayekugusa atapata laana," Sheikh Sharifu alisema huku akitupa kete zake chini.
Lailah alianguka kwa magoti, akilia huku akifungua lile baibui. Chuhu zake zilikuwa zikivuja usaha, na ngozi ya tumbo lake ilikuwa imekunjamana kama ya mwanamke wa miaka tisini. "Nisaidie Sheikh! Nataka kuwa mrembo tena. Nataka kurudi chuo na kuwakomesha wale walionicheka. Nitatoa chochote!"
Mganga huyo alinyamaza kimya kwa muda, kisha akamvuta Lailah karibu na kumnong'oneza neno lililomfanya binti huyo asisimke mwili mzima.
"Dawa ipo. Lakini ili kutoa laana ya mzee wa madini na laana ya mama yako, unahitaji kafara ya damu. Na si damu ya kuku au mbuzi... unahitaji damu ya mtu aliyekubeba tumboni kwa miezi kenda. Unahitaji 'chozi la mwisho' la mama yako."
Lailah alishtuka. "Unamaanisha nimuue mama yangu? Sheikh, mimi ni msalaba, lakini sijafika huko!"
"Chagua, Lailah," Sheikh Sharifu alisema huku akichukua kisu chenye kutu na kukiweka juu ya kioo. "Ubakie hivi, uoze ukiwa hai mpaka funza wakule ukeni na kifuani, au urudishe nyota yako na kuwa mwanamke mwenye nguvu kuliko Tasha na wenzake wote. Mama yako alishakulaani, huna uhusiano naye tena rohoni."
Lailah alitazama vidonda vyake. Alikumbuka dharau za Dr. Makata. Alikumbuka usaliti wa Tasha. Roho yake iliyokuwa imeshajaa sumu ya pombe na ufuska iligeuka kuwa jiwe.
"Nitafanya hivyo," Lailah alisema kwa sauti ya kikatili, macho yake yakiwa mekundu.
Wakati huo huo, kule kijijini Mkanyageni, Mama Lailah alikuwa amelala kitandani, akitweta kwa shida. Ghafla, alianza kupata maumivu makali ya kifua, kama kuna mtu anayemshika koo. Alimwita Kelvin kwa sauti ya chini.
"Kelvin mwanangu... Lailah anakuja. Namuona kwenye giza... anakuja kumaliza kazi aliyoianza," Mama Lailah alinong'ona huku akitokwa na jasho la mauti.
Lailah aliondoka Buguruni usiku ule, akiwa na chupa ndogo ya madawa ya kishirikiana na maelekezo ya kifo. Alikuwa tayari kurudi kijijini, si kwa toba, bali kwa ajili ya kukamilisha kafara itakayomrudishia uzuri wake wa bandia.
---
**Katika Episode inayofuata:**
Lailah anawasili kijijini usiku wa manane. Anakutana na Kelvin mlangoni mwa nyumba ya mama yake. Mapambano makali yanatokea, na Lailah anatumia nguvu za giza alizopewa na mganga. Je, mama yake Lailah atakufa kwa mkono wa binti yake?
**Usikose EPISODE 13: "USIKU WA DAMU MKANYAGENI"**