✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 11: Ukimya wa Ushindi

Baada ya ahadi ile ya bustanini, Kelvin na Briana walianza kuishi kama watu wasiofahamiana. Kelvin alijitolea kikamilifu kufundisha darasa la Kidato cha Nne, akihakikisha anatoa miongozo yote muhimu ya kitaaluma kwa wanafunzi wote, huku akiepuka kabisa kumpendelea Briana au kukaa naye faragha.

Kwa upande mwingine, Briana alibadilika kabisa. Alikuwa wa kwanza kufika darasani na wa mwisho kuondoka. Alitumia kila dakika ya mapumziko kusoma maelezo ya Kelvin na kufanya mazoezi ya mitihani ya nyuma. Macho yake yale ya mahaba sasa yalijawa na mwanga wa akili na bidii. Hakutaka kumwangusha Kelvin, na zaidi ya yote, hakutaka kuipoteza ahadi yao ya baadaye.

Siku ya mtihani wa taifa ilipowadia, Kelvin alikuwa mmoja wa wasimamizi wa nje katika kituo kingine. Aliondoka shuleni hapo bila kumuaga Briana kwa maneno, lakini asubuhi ile alipokuwa akipita kuelekea getini, alimkuta Briana akielekea ukumbi wa mtihani. Macho yao yalikutana kwa sekunde moja. Kelvin alitikisa kichwa kidogo kuashiria "Kila la heri," na Briana alitabasamu kwa ujasiri, kisha akanyanyua kidole gumba juu.

Wiki mbili za mitihani zilipita kama miongo. Kila usiku Kelvin alikuwa akimwombea Briana afanye vizuri. Siku ya mwisho ya mtihani, Briana alimaliza karatasi yake ya mwisho ya somo la Historia, akatoka nje ya ukumbi, na kuvuta pumzi ndefu ya uhuru. Wanafunzi wenzake walikuwa wakishangilia na kuchaniana sare za shule kama desturi, lakini Briana alisimama kando, akitazama upande wa ofisi ya Kelvin iliyokuwa imefungwa.

Alitamani kumuona, kumkumbatia, na kumwambia kuwa amepambana kiume. Lakini alikumbuka onyo la Mkuu wa Shule na ahadi ya Kelvin. Alibeba begi lake, akatoka getini mwa shule, na kuelekea nyumbani kwao, huku akijua kuwa huu ulikuwa mwanzo wa safari ndefu ya kusubiri matokeo yatakayoamua hatima ya penzi lao.

Miezi mitatu baadaye, simu ya Kelvin iliita asubuhi na mapema. Alikuwa ni Mkuu wa Shule.

"Mwalimu Kelvin, matokeo ya Kidato cha Nne yametoka... Unapaswa kuja ofisini kuona kile mwanafunzi wako, Briana, amekifanya. Ni historia!"

**Inaendelea Episode 12...**