✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 1: MKASA WA CD YA AJABU

Ilikuwa ni mwezi wa sita, kipindi cha baridi kiasi, nami nilikuwa likizo ya kidato cha tatu. Nyumbani kwetu kulikuwa na nidhamu ya chuma; mzee alikuwa mtu wa kazi na mama alikuwa muumini kindakindaki wa kanisani. Kitu pekee kilichoruhusiwa kupigwa kwenye deki yetu ni kwaya na taarifa ya habari saa mbili usiku.

Siku hiyo, majira ya mchana, nyumba ilikuwa kimya. Wazazi wako kazini na kanisani, na wadogo zangu wameenda *tuition*. Upweke ulinisukuma kwenda kwa washikaji zangu jirani akina Juma. Kufika pale, nikawakuta wamejifungia, mapazia yameshushwa, macho yao yakiwa yameganda kwenye kioo cha TV.

Walikuwa wanaangalia picha za wakubwa, zile ambazo shuleni tunaziita "warumi." Mapigo ya moyo yalinidunda. Nikawaambia, *"Oya, rudisheni mwanzo nami nione!"* Waligoma. *"Hatuwezi kurudi nyuma, tunamalizia hii tuweke CD ya muziki. Chukua hii CD nenda kacheki kwenu, tutakufuata baadaye tuchukue,"* alisema Juma huku akinikabidhi ile CD ikiwa na mikwaruzo kiasi.

Nilirudi nyumbani kama mwizi. Niliingia sebuleni, nikaangalia huku na kule kuhakikisha hakuna anayeniona. Nikafungua deki, nikaingiza ile CD. Nilikuwa na hamu ya kuona kile ambacho washikaji walikuwa wanakiona. Nilivyoibonyeza tu 'Play', na picha ya kwanza kuanza kutokea...

**PAAAP!**

Giza totoro. Umeme ukakata.

Sauti za washikaji zilisikika nje wakicheka, *"Oyaaa! Umeme huo!"* Lakini kwangu, ule haukuwa umeme kukatika, ilikuwa ni kuanza kwa kifungo. CD ilikuwa ndani ya deki, na deki ile ya kizamani huwezi kutoa kitu mpaka umeme uwake.

Jasho jembamba lilianza kunitoka mdomoni. Niliangalia saa, ilikuwa ni saa kumi jioni. Muda haukusimama. Nilianza kuwaza, ikifika saa mbili usiku umeme ukirudi na Mzee akawasha TV kuangalia habari, nini kitatokea? Je, itatokea picha gani ya aibu mbele ya Mzee?

Nilianza kuhangaika kutafuta bisibisi nifungue deki, lakini mikono ilikuwa inatetemeka kama mtu mwenye degedege. Dunia ilianza kunizunguka...

**ITAENDELEA...**