Episode 3: MTEGO WA TAARIFA YA HABARI SAA MBILI
Hadi inafika saa moja usiku, hali ilizidi kuwa ya hatari. Baba alikuwa amesharudi kutoka kazini, na kama kawaida yake, alikuwa amekaa kwenye kiti chake cha enzi sebuleni, akisubiri umeme urudi ili aangalie taarifa ya habari ya saa mbili usiku.
Giza la sebuleni lilikuwa limegubikwa na mwanga hafifu wa mshumaa uliokuwa mezani. Kila mara niliposikia mlio wa deki ukifanya *"tiktik"*, moyo wangu uliruka. Nilijua umeme ukirudi tu, deki ile ya kizamani ingewaka yenyewe na kuanza kucheza (Auto-play) pale ilipoishia.
*"Mbona leo umeme umechelewa hivi?"* Sauti ya Mzee ilinguruma sebuleni. Alikuwa ameshika rimoti mkononi, akiichezea kama mtu anayesubiri kuanza kwa fainali ya Kombe la Dunia.
Niliwaza haraka. Nilikumbuka mbinu moja ya hatari. *"Baba, leo nahisi nina bidii sana ya kusoma. Naomba nikae hapa sebuleni na madaftari yangu, nimalizie kazi za shule kabla ya kesho,"* nilisema kwa sauti ya upole, nikijifanya kijana mwema sana.
Mzee alinitazama kwa jicho la shaka kupitia mwanga wa mshumaa. *"Sawa mwanangu, elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini ukisikia umeme umerudi, niwashtue mara moja ili niweke habari,"* aliniagiza huku akielekea chumbani kwake kupumzika kidogo.
Niliketi pale sebuleni, madaftari yakiwa wazi, lakini akili yangu ilikuwa kwenye ile deki. Nilianza kutokwa na jasho la hofu licha ya baridi ya mwezi wa sita. Kila mara nilikuwa nanyata kwenda kuangalia taa ya deki kama imewaka.
Muda uliyoyoma... Saa moja na nusu... Saa moja na dakika arobaini na tano... Kila sekunde ilikuwa kama saa nzima.
Ghafla, nilisikia mlio wa redio ya jirani upande wa pili. **UMEME UMERUDI!**
Niliruka kama chui kuelekea kwenye deki, lakini kabla sijafika, nilisikia sauti ya Mama akitokea jikoni: *"Galous! Umeme umerudi, washa TV baba yako asipitwe na habari!"*
Nilipofika mbele ya deki, taa nyekundu ilikuwa imewaka, na kioo kidogo cha deki kikaandika **"READING..."** Moyo ulisimama. Rimoti ilikuwa mkononi mwa Mama aliyekuwa anakuja sebuleni. Nikajua leo ndiyo mwisho wangu.
**ITAENDELEA...**
---
**Episode 4 Inakuja: "SEKUNDE TANO ZA KIFO"**