Episode 6: MBINU ZA SAA TANO USIKU
Nikiwa nimekaa mezani kula chakula cha usiku, kila tonge lilikuwa kama mwiba kooni. Kauli ya Mzee kuwa angeipeleka deki kwa fundi mkuu asubuhi ilikuwa ni hukumu ya aibu mtaani kote. Fundi yule alikuwa mzee wa makuzi na rafiki wa karibu wa Baba—lazima angetoa ripoti kamili ya "uchafu" uliokwama ndani ya mashine.
Mlo wa usiku uliisha kwa ukimya mkubwa. Mama alikuwa akisoma maandiko yake ya kanisani mezani, na Baba alikuwa amesharudi chumbani kwake kusikiliza redio ya mbao iliyokuwa ikipiga nyimbo za kwaya kwa sauti ya chini. Mimi niliaga na kurudi chumbani kwangu, nikijifanya naenda kulala, lakini akili yangu ilikuwa kwenye ile deki iliyokuwa imetulia uvunguni mwa kitanda changu.
*"Lazima nitoe hii CD usiku huu huu, hata kama nitakesha,"* niliwaza huku nikikanyaga taratibu sakafuni ili nisipige kelele.
Saa nne usiku. Nyumba ilitulia tuli. Nilitambaa na kuichukua deki, nikaanza kuifungua skrubu kwa mara ya pili kwa kutumia kisu cha jikoni niliichokuwa nimekiiba wakati wa chakula. Nilifanikiwa kuondoa mfuniko, lakini giza la chumbani lilikuwa adui yangu. Niliwasha kiberiti kimoja baada ya kingine ili nione sehemu ya kutoa ile CD.
Mara, nilisikia mlango wa chumba cha wazazi ukifunguka.
**"Pshiii!"** Nilizima kiberiti haraka na kujitupa kitandani, nikajifunika shuka gubigubi huku deki ikiwa kifuani mwangu.
Mama alichugulia mlangoni. *"Mwanangu, bado hujalala? Naona mwanga wa kiberiti unawaka huku."*
*"Mama, nilikuwa natafuta madaftari yangu ya kesho tuition, nimeshalala sasa,"* nilijibu huku nikijikaza sauti isitetemeke.
Mama alifunga mlango na kurudi kulala. Nilipumua kwa kishindo.
Ilifika saa tano kasoro robo usiku. Niliamua kufanya mbinu ya mwisho ya hatari. Niliichomeka deki kwenye soketi ya chumbani kwangu, nikashikilia kitufe cha *Eject* kwa nguvu, kisha nikawasha swichi ya ukutani.
**"Zzzzz... Clack!"**
Kwa muujiza wa ajabu, deki ilipiga kelele kidogo na lile sinia la CD likatoka nje taratibu!
Moyo wangu uliruka kwa furaha. Niliikamata ile CD kama dhahabu iliyopotea. Haraka sana, niliingiza CD ya kwaya ya akina mama wa kanisani na kuirudisha ndani, kisha nikazima umeme. Nilirudisha mfuniko wa deki, nikakaza skrubu zote, na kuificha ile CD ya aibu katikati ya madaftari yangu ya Fizikia.
Nilijilaza kitandani, nikitokwa na jasho la ushindi. Kesho Mzee anaweza kuipeleka kwa fundi, na fundi akifungua atakuta kwaya ya *"Bwana ni mchungaji wangu."* Nilihisi kama nimevuka daraja la moto.
Lakini, nilisahau kitu kimoja kidogo... Je, asubuhi washikaji zangu wakija kudai CD yao mbele ya Baba, nitawaambia nini?
**ITAENDELEA...**
---
**Episode 7 Inakuja: "MSALA WA ASUBUHI"**