Episode 7: MSALA WA ASUBUHI
Mapambazuko ya saa kumi na mbili asubuhi yalinitikisa. Niliamka nikiwa na uchovu wa kukesha, lakini angalau mzigo wa deki ulikuwa umenitoka kifuani. Nilijua deki sasa ina kwaya, na ile CD ya "warumi" nimeificha vizuri ndani ya daftari la Fizikia, katikati ya mada ya *Electronics*.
Nikiwa bado nimejifunika shuka, nilisikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa. Alikuwa Mzee. Alikuwa ameamka mapema, tayari kwa safari ya kwenda kwa fundi mkuu kabla hajaenda kazini.
*"Mwanangu, ile deki iko wapi? Nipe niiondoshe hapa mapema,"* Mzee aligonga mlango wa chumba changu.
Niliruka kitandani kwa kasi, nikaichukua deki na kumpa mkononi. *"Hii hapa Baba, lakini naona kama niliigusa jana usiku ikakaa sawa. Labda fundi aicheki tu kama 'fuse' haitaleta shida tena."* Nilijikaza kusema kwa upole huku nikijifanya bado nina usingizi.
Mzee aliichukua deki na kuondoka. Nilipumua kwa nguvu. *"Safi sana, sasa niko huru,"* niliwaza.
Lakini nusu saa baadaye, nikiwa bado namsaidia Mama kufagia uwanja, niliona kivuli cha watu wawili kikikaribia getini. Mapigo ya moyo yalianza kudunda tena. Walikuwa ni Juma na mwenzake, washikaji zangu walioniazima ile CD.
*"Oya, mambo vipi?"* Juma alinisalimia huku akitazama huku na kule kuhakikisha Mama hasikii. *"Tuletee ile kitu yetu bwana, jana umeme ulikata tukashindwa kuja kuichukua, sasa hivi tunataka tuipeleke kwa washikaji wengine mtaa wa pili."*
Nilihisi dunia inazunguka. *"Oya, pungeni upepo kwanza! Ile CD haipo hapa,"* niliwanong'oneza kwa ukali.
*"Iko wapi sasa? Usizingue mwanangu, ile CD tumekodi, na tukichelewa kuirudisha tutalipishwa faini ya ziada!"* Juma alianza kupandisha sauti kidogo.
Hapo ndipo Mama alipotoka nje na fagio lake. *"Kuna nini hapa? Akina nani hao mwanangu?"*
Niliwahi kusema: *"Ni marafiki zangu Mama, wanataka madaftari ya Fizikia niliyokuwa nasoma jana usiku."*
Mama alitabasamu. *"Haya, wape madaftari yao waende, wasichelewe tuition."*
Niliingia chumbani mbio, nikachukua lile daftari la Fizikia lenye ile CD ndani yake. Nilikusudia kuwapa daftari zima ili waende nalo mbali na nyumba yetu. Lakini nilipofika mlangoni, niliganda kama nimepigwa na radi.
Mzee alikuwa amerudi! Alikuwa amebeba deki mkononi, na uso wake ulikuwa umekunja kama mtu aliyekasirika sana. Alikuwa ameiweka deki juu ya meza ya barazani mbele ya marafiki zangu.
*"Mwanangu, rudi hapa!"* Mzee aliita kwa sauti ya radi. *"Fundi amesema deki haina tatizo lolote la waya. Lakini amekuta kitu cha ajabu ndani yake ambacho jana ulisema ni 'kwaya'. Juma, nyinyi mmekuja kufuata nini hapa?"*
Niliitazama ile deki, kisha nikatazama lile daftari mkononi mwangu. Siri ilikuwa inakaribia kupasuka mbele ya Mzee, Mama, na washikaji zangu.
**ITAENDELEA...**
---
**Episode 8 Inakuja: "UKWELI KWENYE MEZA"**