✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 4: Majuto ya Msaliti

Chumba cha hoteli kilikuwa kimejaa harufu ya jasho na majuto. Happy alikuwa amejikunyata kwenye kona ya kitanda, huku akijifunika na shuka lililochanika kidogo, mwili wake wote ukiwa unatetemeka. James na Frank walikuwa wanavaa nguo zao kwa utulivu wa kutisha, kana kwamba hakuna kitu cha ajabu kilitokea.

James aligeuka na kumtazama Happy, kisha akatoa simu ya Happy mfukoni mwake na kuitupa juu ya kitanda. "Hiyo hapo simu yako. Nimeifuta namba yangu na ya Frank, na nimehakikisha namba zote ulizokuwa umezizuia (block) nimezifungua."

Happy hakuweza hata kumtazama. Alikuwa akilia kwa kwikwi, sauti yake ikiwa imepotea kwa sababu ya kupiga kelele ambazo hazikupata msaada.

"Sikiliza Happy," James alisema huku akifunga mkanda wake. "Sisi si watu wabaya, ila tumekupa funzo ambalo hutosahau. Ukijaribu kwenda polisi, kumbuka kuwa nina rekodi ya meseji zako zote ukiomba hela kwa uongo na kutapeli watu. Utajifunga mwenyewe kwa utapeli kabla hujatufunga sisi. Hii iwe mwisho wa huu mchezo wako mtaani kwetu."

James na Frank waliondoka chumbani humo na kumwacha Happy akiwa peke yake. Kwa nguvu kidogo alizobaki nazo, Happy alijikokota mpaka bafuni. Kila hatua aliyopiga ilimkumbusha ukatili aliopitia. Alijitazama kwenye kioo na kushindwa kujitambua; macho yamevimba, nywele zimevurugika, na utu wake umepotea.

Alijilaza kwenye sakafu ya bafuni na kulia kwa uchungu. Alimkumbuka Juma, mpenzi wa Asha, ambaye alikuwa akimcheka kila siku kwa sababu hana pesa. Alimkumbuka Asha aliyemwambia kuwa "malipo ni hapa hapa duniani."

Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, Happy alijikokota na kuvaa nguo zake zilizokuwa zimechanika sehemu chache. Alitoka hotelini hapo kama mwizi, akijifunika uso wake kwa mtandio. Alipofika mtaani kwao, alimkuta Asha amekaa nje, macho yake yakiwa mekundu kwa kukosa usingizi.

Asha alipomuona Happy, alikimbia kumlaki. "Happy! Mungu wangu, umepatwa na nini?"

Happy alishindwa kusema neno. Alimwangukia Asha na kuanza kulia kwa nguvu. Asha alimpeleka ndani haraka na kumstiri. Baada ya kumpa maji na kumtuliza, Happy alisimulia kila kitu kilichotokea.

Asha alikuwa amepigwa na butwaa. Ingawa alikuwa akimuonya Happy, hakutarajia kuwa yangefika huko. "Pole sana Happy. Lakini nakuomba, sasa hivi ndio wakati wa kubadilika. Hizi hela za nauli hazijawahi kumtajirisha mtu, zinaishia kwenye aibu tu."

Happy akatikisa kichwa. "Asha, nimejifunza. Sitaki tena kusikia habari za wanaume, wala sitaki tena kugusa hela ya mtu kwa ujanja. Naumia sana Asha, naumia mwili na roho."

Lakini wakati Happy akifikiria kuanza maisha mapya, huko nje Juma alikuwa anakuja na habari nyingine mbaya. Alikuwa amesikia tetesi mtaani kuwa kuna "mla nauli mmoja amekamatwa na kufundishwa adabu hotelini." Juma alikuwa anakuja kutaka kujua kama ni kweli ni Happy, bila kujua kuwa hili jambo lingeweza kuleta mpasuko mkubwa zaidi kati yake na Asha.

---
**ITAENDELEA...**