Episode 5: Siri Kufunuka
Asha alikuwa bado anamsaidia Happy kusafisha majeraha yake huku akimfariji kwa maneno ya imani, mara mlango wa chumba chao ukagongwa kwa nguvu. Happy alishtuka na kujikunyata pembeni mwa kitanda, hofu ikimrudia upya akidhani labda James amerudi kumalizia alichokianza.
"Happy! Asha! Fungueni mlango, ni mimi Juma!" sauti ya Juma ilisikika kwa ukali nje ya mlango.
Asha alimtazama Happy kwa wasiwasi kisha akaenda kufungua mlango. Juma akaingia ndani kwa haraka, macho yake yakiwa yamepanuka. Hakumtazama hata mpenzi wake Asha, macho yake yalielekea moja kwa moja kwa Happy ambaye alikuwa amejifunika kwa shuka huku akijaribu kuficha uso wake.
"Kumbe ni kweli!" Juma alisema kwa sauti ya dhihaka. "Mtaani kote sasa hivi habari ni moja tu. Kwamba mla nauli maarufu wa mtaa huu amepatwa na dhoruba hotelini. Happy, kumbe ulikuwa unajifanya mjanja, leo umegeuka kuwa kitoweo cha watu wawili kwa mpigo?"
Asha alimkamata mkono Juma, akijaribu kumtuliza. "Juma, tafadhali nyamaza! Huoni mwenzako ana maumivu? Hii siyo saa ya kumdhihaki, ni saa ya kumpa pole."
Juma alimshika Asha mabega na kumtikisa kidogo. "Pole ya nini Asha? Huyu rafiki yako alikuwa anakucheka kila siku kwa sababu wewe unaniheshimu mimi. Alikuwa anakuona wewe mshamba kwa sababu huli nauli za watu. Leo Mungu amemlipa kwa ujeuri wake, wewe bado unampa pole?"
Happy alijikaza na kunyanyua kichwa, sauti yake ikiwa imeparara. "Juma, ni kweli nimekosea na nimepata adhabu yangu. Lakini kwanini unajisikia furaha kuona nimeumizwa hivi? Je, na wewe ulikuwa mmoja wa wale waliokuwa wanapanga kuniumiza?"
Juma alicheka kicheko cha kejeli. "Mimi? Mimi sina hela ya kupoteza kutuma nauli kwa mwanamke kama wewe. Lakini nakuambia ukweli, James ni rafiki yangu wa karibu sana wa kazini. Jana usiku aliniambia kila kitu. Aliniambia jinsi ulivyokuwa unajivuta na kujidai, mpaka ulipoanza kuomba msamaha kwa magoti."
Asha aliposikia maneno hayo, alipigwa na butwaa. Alimwachia Juma na kusogea nyuma hatua mbili. "James ni rafiki yako, Juma? Na ulijua mpango wote uliokuwa unaendelea? Na hukuniambia mimi ili nimzuie Happy asitoke?"
Juma alijaribu kujitetea, "Asha, huyu rafiki yako alihitaji kufundishwa adabu. Angeendelea hivi angekuja kukuponza na wewe."
"Hapana Juma!" Asha alifoka huku machozi ya hasira yakimtoka. "Hata kama Happy alikuwa na makosa, ukatili aliofanyiwa haustahili mwanamke yeyote. Kama James ni rafiki yako na mlishirikiana kupanga haya, basi wewe si mwanaume niliyedhani nimekupa moyo wangu. Wewe ni mkatili kama wao!"
Mvutano ulikuwa mkubwa ndani ya kile chumba kidogo. Happy alijiona kuwa chanzo cha ugomvi wa mpenzi wake na rafiki yake wa pekee. Lakini katikati ya ule ugomvi, simu ya Juma ilianza kuita. Alipoitazama, akashtuka. Alikuwa ni Pili Kiswaswadu, mwanamke mwingine wa mtaani ambaye alijulikana kwa tabia za ushindani na Asha.
"Kwanini Pili anakupigia simu saa hizi?" Asha aliuliza kwa sauti ya kutilia shaka, akimnyang'anya Juma simu kabla hajapokea.
Siri nyingine ilikuwa inakaribia kuchomoza, siri ambayo ingeweka wazi kuwa si Happy tu aliyekuwa anaishi maisha ya uongo mtaani hapo.
---
**ITAENDELEA...**