Episode 8: Anguko la Juma na Kimbunga cha Polisi
Baada ya maneno ya James, mtaa mzima ulikumbwa na ukimya wa ajabu. Pili Kiswaswadu, ambaye sekunde chache zilizopita alikuwa akipayuka kwa dharau, alianza kutetemeka. Wazo la Juma kukamatwa kwa wizi na uwezekano wa yeye kuhusishwa kama mnufaika wa hizo hela lilimfanya aanze kutafuta upenyo wa kutokomea.
"James, mimi sijui chochote kuhusu wizi wa Juma!" Pili alijitetea huku akijaribu kurekebisha kanga yake iliyovurugika kwenye timbwili. "Yeye alikuwa ananiletea hela tu, sikuwa nauliza anazitoa wapi!"
James alimtolea macho ya ukali. "Utajieleza huko mbele. Polisi wapo njiani kuja hapa kwa sababu Juma amekiri kuwa vifaa vingine alivificha kwako ili usiviuze mpaka bei ipande. Wewe ndiye uliyekuwa unamshinikiza atafute hela kwa gharama yoyote."
Asha alijiegemea ukutani, akijisikia mwenye bahati kwa kumfukuza Juma mapema. "Mungu ni mwema," alijisemea moyoni. "Lau nisingegundua usaliti wake leo, ningekutwa na haya majanga ndani ya chumba changu."
Ghafla, ving'ora vya polisi vilisikika kwa mbali vikikaribia. Pili alipisikia vile ving'ora, akili ikamruka. Aligeuka na kuanza kukimbia kuelekea uchochoroni, lakini kutokana na haraka na kanga yake kuwa mbovu, alijikwaa na kuanguka vibaya mbele ya gari la James.
Dakika chache baadae, gari la polisi liliingia uwanjani. Askari watatu walishuka, mmoja akiwa amemshika Juma ambaye alikuwa amepigwa pingu, uso wake ukiwa umejaa damu na mavumbi, akionyesha dhahiri kuwa "shughuli" ilikuwa pevu huko alikotoka.
"Ndiye huyu?" Askari mmoja alimuuliza James huku akimnyooshea kidole Pili aliyekuwa akijikokota chini.
"Ndiye huyo, na huyo mwingine mlangoni ndiye Happy," James alijibu kwa sauti ya baridi.
Happy alishtuka. "Mimi? James, mimi nimehusika nini na wizi wa Juma?"
Askari alimsogelea Happy. "Juma amesema kuwa sehemu ya hela alizokuwa akiziiba, alikuwa anakutumia wewe kama 'nauli' ili usitoe siri zake za uhusiano na Pili. Kwamba ulikuwa unamtishia kumwambia Asha kama asipokupa hela. Kwa hiyo wewe pia ni mnufaika wa mali ya wizi."
Happy alihisi dunia inamzunguka upya. Adhabu ya James na Frank hotelini haikutosha? Sasa na gerezani? "Hapana afande! Mimi nilikuwa nakula nauli tu kama mchezo wangu wa kawaida, sikujua kama ni hela za wizi! James, tafadhali nisaidie!"
James aligeuza uso. "Happy, nilikuambia leo kila mtu abebe msalaba wake. Ulidhani kula jasho la watu ni sifa, sasa kula na jasho la wizi uone chungu yake."
Polisi waliwashika Pili na Happy na kuwapandisha kwenye difenda la polisi. Juma alikuwa ameinama kwa aibu, akishindwa hata kumtazama Asha ambaye alikuwa amesimama mbali akishuhudia wapenzi wake wa zamani na rafiki yake wakichukuliwa.
Mtaa mzima ulikuwa umejaa watu wakizomea. "Wala nauli hao! Wezi hao! Malaya hao!" maneno yale yalimchoma Happy kuliko viboko alivyowahi kupata.
Asha alibaki amesimama peke yake uwanjani huku difenda likiondoka kwa kasi na vumbi jingi. James alimsogelea Asha na kumtazama kwa huruma. "Asha, wewe ni mwanamke mzuri na mwenye msimamo. Usiruhusu uchafu wa hawa watu ukuchafue na wewe. Anza maisha yako upya, na uwe makini na watu unaowaita marafiki."
James alipanda gari lake na kuondoka. Asha alirudi ndani ya chumba chake, akakifunga kwa ufunguo, na kuanguka kitandani. Mtaa ulikuwa mkimya sasa, lakini moyo wake ulikuwa na dhoruba kubwa. Siri moja ilikuwa imefunika nyingine, na safari hii, mchezo wa "Mpenda Pumbu Hali Nauli" ulikuwa umezalisha msiba wa kijamii.
---
**ITAENDELEA...**