Episode 14: HARUFU YA KISASI NA SAUTI YA HAKI
Ndani ya kachumba kile kidogo cha Erica, Jonas alikuwa akisikia kila neno lililokuwa likizungumzwa nje. Harufu ya udi iliyokuwa ikitoka kwenye nguo za Erica zilizotundikwa ukutani ilimfanya ajihisi kama ananyongwa. Kila mara alipovuta pumzi, alihisi kama mtego wa mauti unazidi kukaza shingoni mwake.
Nje ya mlango, Bibi Maria alikuwa amesimama imara mbele ya askari wawili waliokuwa wameshika tochi kubwa na silaha.
"Bibi, tunakuuliza tena," askari mmoja alisema huku akimulika tochi ndani ya sebule ile ndogo. "Kuna mwanamume yeyote amepita hapa? Tuna ushahidi kuwa mhalifu aliyekimbia Arusha ana majeraha na ameelekea upande huu."
Jonas alifumba macho, mikono yake ikitetemeka huku akishika bahasha ya mamilioni ya fedha ambayo sasa ilionekana kama karatasi chafu. Alitega sikio kusikia jibu la Bibi Maria.
"Afande," Bibi Maria alianza kusema, sauti yake ikiwa tulivu lakini yenye uzito wa ajabu. "Mimi ni mzee, na mjukuu wangu amefariki leo hii. Nyumba hii imejaa huzuni, si mhalifu. Kama kuna mtu amepita, labda ameelekea kule bondeni kwenye mashamba ya kahawa."
Askari wale walitazamana. "Basi sawa bibi, pole kwa msiba. Lakini tukigundua unamficha, sheria haitakuacha salama."
"Mungu ndiye anayejua siri za kila nyumba," Bibi Maria alijibu kwa mafumbo.
Ving'ora vilianza kusikika kwa mbali vikitoka eneo lile kuelekea bondeni. Jonas alishusha pumzi ndefu, akijiona kama amepata nafasi ya pili ya kuishi. Lakini furaha yake ilikuwa ya muda mfupi. Mlango wa chumba chake ulifunguka kwa fujo, na Bibi Maria akaingia akiwa ameshika taa ya chemli, uso wake ukiwa na giza la kutisha.
"Nimekuokoa kwa polisi, lakini sijakuokoa kwangu," Bibi Maria alinong'ona.
Jonas alijaribu kusimama. "Bibi, asante sana! Hizi pesa chukua zote, nitaondoka sasa hivi na kukuachia maisha ya anasa."
Bibi Maria alizipiga zile pesa kwa mkono mmoja, zikatawanyika sakafuni kama majani makavu. "Pesa hizi haziwezi kumrudisha Erica! Nimegundua wewe ni nani tangu ulipoingia hapa. Harufu ya damu yako inafanana na harufu ya machozi ya mjukuu wangu."
Bibi Maria alimsogelea Jonas, taa ya chemli ikimulika macho yake yaliyokuwa na cheche za hasira. "Ulimvua chupi Erica kwa ahadi ya ajira. Ulimfanya ajione takataka mpaka akaamua kunywa sumu. Sasa, nimeamua... hutatoka ndani ya chumba hiki mpaka utakapolipia kila tone la machozi alilolila."
Ghafla, Jonas alihisi mwili wake ukianza kulegea. Alijaribu kutoa sauti lakini ulimi ulimvimbia. Alikumbuka kile kinywaji cha chai ya kienyeji alichopewa na Bibi Maria muda mchache uliopita.
"Umenipa nini?" Jonas aliuliza huku akianguka polepole kwenye kitanda cha Erica.
"Dawa ya kienyeji ya kumfanya mnyama atulie," Bibi Maria alisema huku akitoka nje na kufunga mlango kwa lock nzito ya chuma. "Leo usiku, utazungumza na kivuli cha Erica mpaka asubuhi itakapochomoza na sheria kukuchukua."
Jonas alibaki gizani, mwili ukiwa umepooza, huku akianza kuona maono ya Erica akimtokea pembeni ya kitanda, akicheka kicheko cha kutisha huku akimnyooshea kidole. Adhabu ya kweli ilikuwa imeanza.
**INAENDELEA SEHEMU YA 15...**