Episode 15: MAONO YA KABURI NA SAUTI ZA DHAMBI
Giza la chumba cha Erica lilikuwa zito kama shubiri. Jonas alikuwa amelala chali kwenye kile kitanda cha kamba, huku mwili wake ukiwa kama umepigwa ganzi ya mauti. Dawa ile ya Bibi Maria ilikuwa imemkamata sawasawa; hakuweza kunyanyua hata kidole, lakini milango yake ya fahamu ilikuwa wazi zaidi ya kawaida. Alikuwa mfungwa ndani ya mwili wake mwenyewe.
Harufu ya udi ilianza kubadilika. Haikuwa tena harufu ya manukato ya kike, bali ilianza kunuka harufu ya udongo mbichi wa kaburi. Jonas alihisi baridi kali ikipanda kuanzia miguuni mwake.
*“Jonas...”* Sauti nyembamba ilinong’ona sikioni mwake. Jonas alijaribu kugeuza kichwa lakini hakuweza. Moyo wake ulidunda kwa fujo kifuani kama unataka kupasuka. Katika kona ya chumba, mwanga hafifu wa kijani ulianza kutokea, na polepole, kivuli cha mwanamke kikajitokeza.
Alikuwa ni Erica. Alikuwa amevaa gauni lilelile jekundu alilokuwa nalo siku ya kwanza Jonas alipomvua utu wake. Lakini uso wake haukuwa na tabasamu; ulikuwa na makovu ya sumu iliyounguza midomo yake, na macho yake yalikuwa mekundu kama makaa ya moto.
*“Ahadi ya ajira iko wapi, Jonas?”* Erica aliuliza, akimsogelea kitandani. Sauti yake ilikuwa inasikika kama mchanga unavyosuguliwa kwenye bati. *“Uliniahidi maisha ya anasa, ukaniambia nikupe kila kitu changu... sasa mimi niko chini ya ardhi, na wewe uko hapa kwenye kitanda changu.”*
Jonas alitaka kupiga kelele, alitaka kuomba msamaha, lakini kinywa chake kilikuwa kimefungwa na nguvu asiyoijua. Erica alinyoosha mkono wake uliokuwa na baridi ya barafu na kuugusa uso wa Jonas. Jonas alihisi maumivu makali, kama anachomwa na pasi.
*“Leo nimekuja kuchukua mkataba wangu, Jonas. Mkataba wa damu,”* Erica alinong’ona huku akizidi kumkaribia mpaka nyuso zao zikakaribiana.
Wakati huohuo, kule sebuleni, Bibi Maria alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha mbao, akisali kwa sauti ya chini huku akishika picha ya mjukuu wake. Machozi yalikuwa yakimtiririka. Neema alikuwa amesimama mlangoni, akisikiliza vilio vya chini vilivyokuwa vikitoka ndani ya chumba cha Erica — vilio vya Jonas aliyekuwa anapambana na mizimu ya matendo yake.
“Mama, hatutamdhuru zaidi?” Neema aliuliza kwa sauti ya hofu.
“Haki haina haraka, mwanangu,” Bibi Maria alijibu bila kugeuka. “Mungu amemleta hapa ili ajionee mwenyewe kile alichokipanda. Alfajiri ikifika, tutamkabidhi kwa mikono ya sheria. Lakini kwa usiku wa leo, atakuwa mgeni wa Erica.”
Ndani ya chumba, Jonas alikuwa akiona maono ya wasichana wengine wote aliowadhalilisha. Halima, Sada, na wengineo walikuwa wamemzunguka, kila mmoja akimvuta kwa nguvu kuelekea kwenye shimo jeusi lililokuwa likifunguka chini ya kitanda. Alikuwa akipitia jehanamu kabla hata hajafa.
“Nisameheni... nisameheni...” Sauti ile ilirindima kichwani mwake, huku akizama zaidi kwenye giza la usiku ule wa malipo.
**INAENDELEA SEHEMU YA 16...**