Episode 8: MZIMU WA ERICA NA MLANGO WA JEHANAMU
Jonas aliingia ndani ya lango la ofisi za Terejo huku akiwa amevaa miwani meusi na kofia iliyofunika nusu ya uso wake. Alihisi kila jicho la mlinzi na mfanyakazi lilikuwa likimchoma kama msumari wa moto. Hakuwa tena yule mkurugenzi aliyekuwa akitembea kwa madaha na harufu ya pafyumu ghali; sasa alikuwa ni kivuli cha mtu aliyepotea.
Alipofika mlangoni mwa ofisi ya Mzee Kimario, alikuta milango ikiwa wazi. Ndani kulikuwa na askari wawili wa kanzu na mwanamke mmoja aliyekuwa ameketi akilia kwa kwikwi. Jonas alipokaribia, moyo wake ulistuka — hakuwa Erica, bali alikuwa ni mama yake mzazi Erica.
"Huyu hapa amekuja," Mzee Kimario alisema kwa sauti ya baridi, akimnyooshea kidole Jonas.
Askari mmoja alinyanyuka na kumsogelea Jonas. "Jonas, unapaswa kuandamana nasi kituo cha polisi. Lakini kabla ya hapo, unapaswa kujua kuwa Erica hayupo tena duniani. Amefariki saa moja lililopita hospitalini baada ya kunywa sumu kali ya kusafishia vyoo."
Jonas alihisi kama radi imepiga ndani ya chumba kile. "Amekufa? Kwa nini?"
Mama yake Erica alinyanyuka na kumrukia Jonas, akimvuta shati kwa nguvu huku akipiga kelele. "Mnyama wewe! Mwanangu ameacha barua... amesema ulimgandamiza, ukamvua utu wake kwa ahadi ya kazi ambayo hukumkatalia wala kumpa. Alishindwa kuvumilia aibu ya kile ulichomfanyia!"
Askari walimtuliza yule mama, lakini maneno yake yalikuwa kama hukumu ya mwisho kwa Jonas. Polisi mmoja alimvuta Jonas pembeni na kumnong'oneza, "Barua ya Erica inasema pia alidanganya kuhusu kuwa na UKIMWI ili kukulipa kisasi cha kile ulichomfanya. Alijua hofu ya kifo ingekutesa zaidi kuliko jela. Lakini sumu aliyokunywa ndiyo imekatisha maisha yake kweli."
Jonas alihisi ganzi mwili mzima. Kwa upande mmoja, alihisi nafuu kwamba labda hana virusi vile, lakini kwa upande mwingine, damu ya Erica ilikuwa mikononi mwake. Alikuwa amesababisha kifo cha binti mdogo kwa tamaa zake za kinyama.
"Jonas," Mzee Kimario aliingilia kati, sauti yake ikiwa na chuki ya dhahiri. "Kifo cha Erica kimeleta uchunguzi mkubwa. Akaunti za ofisi zimefungwa, na kila miamala uliyofanya inakaguliwa. Polisi wamegundua ulikuwa unatumia fedha za kampuni kuwahonga wasichana warembo."
Jonas alijua huu ndio wakati wa mwisho. Alitazama nje ya dirisha na kuona gari la polisi likiwa limepaki. Akili yake ilianza kufanya kazi kwa kasi ya ajabu. Alikumbuka funguo za gari ya ofisi zilizokuwa mfukoni mwake, na bahasha ya fedha taslimu aliyokuwa ameificha kwenye droo yake ya siri asubuhi ile.
"Naomba... naomba niende msalani mara moja," Jonas aliomba kwa sauti ya unyonge, akijifanya kama anataka kutapika tena.
Askari walitazamana, kisha mmoja akamruhusu. "Haya nenda, lakini usichelewe."
Jonas alitoka nje ya ofisi kwa kasi, lakini badala ya kuelekea msalani, alipita mlango wa dharura wa nyuma. Alikimbia kuelekea sehemu ya kuegesha magari, akawasha injini ya gari ya ofisi kwa fujo na kupiga reva iliyopiga kelele ya tairi barabarani. Alijua akishikwa sasa, hatatoka jela maisha yake yote.
Safari ya kutoroka ilikuwa imeanza, huku sauti za ving'ora vya polisi zikianza kusikika kwa mbali nyuma yake.
**INAENDELEA SEHEMU YA 9...**